Mwongozo wa Kuchagua Kompyuta Bora kwa Kazi za Graphics Design

Mwongozo wa Kuchagua Kompyuta Bora kwa Kazi za Graphics Design

Kama unafanya kazi za graphics design, kuchagua kompyuta sahihi ni muhimu sana. Kompyuta mbovu inaweza kufanya kazi zako kuwa ngumu na kuchelewesha projects.
Hapa nakuonesha madaraja matatu ya kompyuta: sifa za chini, za kati na za juu, pamoja na mifano na makadirio ya bei zake.

Hii ni kwa wale wanaoanza kujifunza au wana bajeti ndogo. Inafaa kwa kazi nyepesi kama Photoshop, Illustrator, au Canva.

Sifa za lazima:

  • Processor: Intel Core i5 (Gen 8 au zaidi) au AMD Ryzen 5
  • RAM: 8GB
  • Storage: 256GB SSD
  • Graphics Card: Integrated Graphics (Intel UHD au AMD Radeon Vega)
  • Screen: 14″-15.6″ Full HD

Mifano:

  • Acer Aspire 5 (Intel Core i5, 8GB RAM, 256GB SSD)
  • Lenovo IdeaPad 3 (AMD Ryzen 5, 8GB RAM, 256GB SSD)

Hii ni kwa mtu anayefanya design mara kwa mara, anatumia programu nyingi kwa wakati mmoja kama Photoshop, Illustrator, na Adobe XD.

Sifa za lazima:

  • Processor: Intel Core i7 (Gen 10 au zaidi) au AMD Ryzen 7
  • RAM: 16GB
  • Storage: 512GB SSD
  • Graphics Card: Dedicated Graphics (NVIDIA GTX 1650 au AMD Radeon RX 5500M)
  • Screen: 15.6″ Full HD IPS

Mifano:

  • Dell Inspiron 15 5000 (Intel Core i7, 16GB RAM, GTX 1650)
  • HP Pavilion Gaming 15 (Ryzen 7, 16GB RAM, GTX 1650)

Makadirio ya bei:
Tsh 2,000,000 hadi Tsh 2,900,000

Hii ni kwa mtu anayefanya kazi kubwa kama video editing, 3D rendering, au heavy graphics design projects.

Sifa za lazima:

  • Processor: Intel Core i7/i9 (Gen 12 au zaidi) au AMD Ryzen 9
  • RAM: 32GB au zaidi
  • Storage: 1TB SSD
  • Graphics Card: NVIDIA RTX 3060/3070 au AMD Radeon RX 6800M
  • Screen: 15.6″ au 17.3″ 2K au 4K IPS

Mifano:

  • MacBook Pro 16″ M2 Pro (32GB RAM, 1TB SSD)
  • Dell XPS 15 (Intel Core i9, 32GB RAM, RTX 4070)
  • Asus ROG Strix G16 (Intel Core i9, RTX 4070, 32GB RAM)

Makadirio ya bei:
Tsh 5,500,000 hadi Tsh 9,500,000

        • Kama unafanya kazi mara kwa mara, chagua daraja la kati.
        • Kama unajifunza tu au bajeti ni ndogo, daraja la chini linakutosha.
        • Kama wewe ni professional au unafanya kazi nzito, daraja la juu ni sahihi.

        Kumbuka:
        SSD na RAM ni muhimu sana kwa kasi ya kompyuta yako. Usichague kompyuta yenye HDD pekee bila SSD.

        Shopping Cart