Mambo Ma 5 ya Kushangaza Kuhusu Logo

Mambo Ma 5 ya Kushangaza Kuhusu Logo

Nembo (logo) ni alama rahisi lakini yenye nguvu kubwa. Inawakilisha chapa, hujenga imani, na mara nyingine hubeba siri ambazo wengi hawazijui. Hapa kuna mambo matano ya kushangaza kuhusu logo ambazo huenda hukuwahi kufikiria.

Nembo ya zamani zaidi ambayo bado inatumika ni ya Stella Artois, kampuni ya bia kutoka Ubelgiji. Ilianza kutumia nembo hiyo tangu 1366 – zaidi ya miaka 650 iliyopita! Nembo hiyo ina picha ya goblet (kombe la bia) na imebadilika kidogo sana kwa miaka mingi, ikithibitisha kuwa nembo bora hudumu na huacha alama ya kudumu.

Watu wengi hudhani logo nzuri lazima iwe na gharama kubwa – lakini si mara zote. Angalia mifano hii:

  • Nike: Logo ya “swoosh” ilitengenezwa kwa $35 tu mwaka 1971 na mwanafunzi wa design, Carolyn Davidson. Baadaye, alipewa hisa za kampuni kama shukrani.
  • Pepsi: Mwaka 2008, Pepsi ililipia zaidi ya $1 milioni kubuni logo mpya kupitia shirika la design, Arnell Group.
  • BBC: Iliweka zaidi ya £1.8 milioni kubadili logo yao mwaka 2021, huku mabadiliko yakiwa madogo sana.

Gharama ya logo inaweza kuwa ndogo au kubwa, lakini thamani yake huwa kubwa zaidi ikiwa inawakilisha chapa vyema.

Logo ya NIKE iliwagharimu nike kiasi cha $ 35, sawa na TSH 94,000

Wabunifu wa logo mara nyingi huficha ujumbe, maana, au picha ndani ya nembo:

  • FedEx: Kuna mshale kati ya herufi E na x, unaoonyesha kasi na mwelekeo.
  • Amazon: Mshale unaonyesha kutoka a hadi z, ukimaanisha wanauza kila kitu. Pia, unafanana na tabasamu.
  • Toyota: Mduara kwenye logo yao unaweza kutengeneza herufi zote za “Toyota”.

Pepsi na Coca-Cola wamekuwa kwenye ushindani wa chapa kwa zaidi ya karne moja. Coca-Cola imehifadhi fonti yake ya kipekee tangu mwaka 1887. Wakati huo huo, Pepsi imebadili logo yake zaidi ya mara 10.

  • Coca-Cola ina nembo yenye hisia za kihistoria, uaminifu, na utulivu.
  • Pepsi hujaribu kuwa ya kisasa, inayobadilika kulingana na kizazi.

Lakini, tafiti nyingi zinaonyesha watu hukumbuka Coca-Cola zaidi kwa sababu ya uthabiti wa nembo yao.

Logo ya Lacoste ina mamba kwa sababu ya mchezaji wa tenisi René Lacoste aliyekuwa na jina la utani “The Crocodile”. Alitengeneza fulana za michezo zenye logo hiyo, na hazikupendwa mwanzoni.

Kwa miaka ya 1930, kuvaa nguo yenye logo ilikuwa kama kucheza kamari – haikuwa ya kawaida. Lakini leo, Lacoste ni mojawapo ya chapa maarufu duniani. Wazo la kuweka mnyama kama nembo liliwafanya wasimame tofauti sokoni. Mbunifu wa mavazi anaweza kutumia Illustrator kuunda michoro ya mavazi kwa ajili ya kiwanda cha nguo.

Hitimisho
Logo si tu picha. Ni hadithi, ni historia, na wakati mwingine ni siri. Kila nembo nzuri huwasiliana zaidi ya macho yanavyoona. Ukiona logo tena, jiulize: “Ina nini kingine kisichoonekana kirahisi?

Je, ungependa kujifunza zaidi kuhusu kila hatua katika kubuni na ku design logo au nembo? Angalia hii


Shopping Cart