
Hupanua Fursa za Kazi na Michongo
Ujuzi wa Motion graphics unakufanya kuwa Designer mwenye thamani zaidi. Waajiri na wateja wengi wanapendelea Designers wanaoweza kufanya kazi za Static Graphics na Motion graphics(Animated).
Pia kuna uhitaji mkubwa sana wa Motion Graphics designer kwa sababu Social Media, Media houses e.g TV Stations, zinahitaji zaidi maudhui ya videos.
Huongeza Kipato chako
Wabunifu(Designer) wa Motion graphics hulipwa zaidi kuliko wale wa Static Graphics. Ukiwa na ujuzi huu, unaweza kutoza zaidi kwa kazi zako na kuvutia Project kubwa zaidi.
Kujitenga dhidi ya Ushindani
Tafiti zinaonesha dunaini kote ni 10-20% ya Graphics designer duniani kote ndiyo wanafanya Motion Graphics. Waliobaki wote wanafanya Static design. Hii inamaanisha ukiwa Motion Graphics designer unajitenga na ushindani katika masoko na kazi.
Hitimisho
Motion graphics ni moja ya ujuzi wa ubunifu unaokua kwa kasi zaidi kutokana na mahitaji makubwa katika masoko ya kidijitali, mitandao ya kijamii, na matangazo.
Traditional graphic designers wengi kwa sasa wanajifunza Motion graphics ili kuendelea kuwa na ushindani.